HAYA NDIO MAAZIMIO BAADA YA KIKAO CHA WACHEZAJI WA ZAMANI WA YANGA

Wachezaji wa zamani wa klabu ya Yanga leo hii wamekutana na makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga na kufanikiwa kupanga mipango mbalimbali inayohusiana na klabu hiyo hasa kutoka kwao wachezaji hao.

Katika kikao hicho maazimio yaliyowekwa ni pamoja na,
1.Kuwashirikisha katika masuala ya klabu na kuwaweka karibu na klabu.

2.Kujenga umoja wa wana Yanga kwa ujumla.

3.Kuunda safu ya uongozi wao itakayorahisisha mawasiliano baina yao na uongozi wa klabu.

4.Kuweka kumbu kumbu kwaajili ya historia ya klabu na vizazi vijavyo kupitia wao.

5.Kusaidiana katika suala zima la ugunduzi wa vipaji vya wachezaji kwa manufaa ya klabu.

Wakati huo Sanga amejaza nafasi mbili za wajumbe wa kamati ya utendaji zilizokuwa wazi na moja iliyoachwa na mjumbe aliekuwa mwenyekiti wa kamati ya mashindano Mhandisi Malume ambae yeye alienda nje ya nchi kwa ajili ya masomo.

Wajumbe walioteuliwa na makamu mwenyekiti kujaza nafasi hizo ni,
-Mr.Mohamed Nyenge
-Mr. Tonny Mark
-Mr.Majid Suleiman.


Maamuzi hayo ya kuteua wajumbe yamefanyika kwa mujibu wa kikao cha kamati ya utendaji kilichokaa tarehe 15 mwezi wa saba mwaka huu na pia kwa mujibu wa katiba ya 28:(1)d ambayo inaeleza kuwa mwenyekiti ana mamlaka ya kujaza nafasi mbili za wajumbe wa kamati ya utendaji.

No comments