ERASTO NYONI AJIUNGA NA KLABU YA SIMBA

Klabu ya Simba bado inaendelea na harakati zake za usajili baada ya leo hii kukamilisha usajili wa mchezaji Erasto Nyoni ambae awali alikuwa anaitumikia timu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani mkoani Morogoro.

Klabu ya Simba imethibitisha kumpa kandarasi ya miaka miwili Nyoni kwa ajili ya kujiunga na wekundu hao wa msimbazi ambao wanataraji kuiwakilisha nchini katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Awali Nyoni alikuwa anahusishwa na taarifa za kujiunga na klabu ya Yanga baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa uongozi wa Yanga ulikuwa na nia ya kumpa mkataba wa kuitumikia Yanga.

No comments