SINGIDA UNITED YAMALIZANA NA DEUS KASEKE

Timu ya Singida United imefanikiwa kukamilisha usajili wa mchezaji wa timu ya Yanga Deus Kaseke,baada ya mchezaji huyo kusaini kandarasi ya miaka miwili kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo iliyopanda daraja kucheza ligi kuu ya Tanzania bara.
Kaseke amejiunga na klabu ya Singida United kama mchezaji huru baada ya mkataba wake na klabu ya Yanga kumalizika.

Hata hivyo Yanga ilishindwa kumuongezea mkataba mpya baada ya kushindwana kwenye masuala ya kimaslahi.

Singida United ni miongoni mwa vilabu ambavyo vinatazamwa na wadau wengi wa soka wakiamini kwamba huenda wakaleta ushindani wa hali ya juu,hii inatokana na mipango yao ya kiundeshaji huku ikifanikiwa kusajili wachezaji mahili kutoka nchi mbalimbali.

No comments