YANGA WATAMBA KULINYAKUA TAJI KWA MARA YA NNE

Uongozi wa timu ya Yanga umejinasibu kufanya vizuri katika msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara hii inatokana na maandalizi ambayo wanayafanya.

Afsa Habari msaidizi wa timu hiyo,Godlisten Anderson Chicharito alisema kwamba jana kikosi kilimaliza mazoezi ya Gym na wachezaji wamepewa mapumziko ya siku mbili kabla ya kurejea kuendelea na mazoezi ya uwanjani yatakayofanyika kwenye uwanja wa Uhuru.

Alisema kwamba dhamira yao ni kuchukua taji la ligi kuu kwa mara ya nne mfululizo kwani anaamini hakuna timu ambayo itawazuia kufanya hivyo.

Chicharito alisema kwamba katika kujiweka sawa na maandalizi kikosi hicho pia kinataraji kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Singida United,mchezo unaotarajiwa kupigwa agost 5 mwaka huu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

No comments