MINZIRO AUSHANGAA UONGOZI WA SINGIDA UNITED

Aliyekuwa kocha msaidizi wa timu ya Singida United,Fredrick Minziro amesema kwamba uongozi wa timu hiyo ndio umeamua kuachana nae licha ya yeye kuwa miongoni mwa makocha walioipandisha timu.

Minziro alisema kwamba awali alikuwa kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba na uongozi huo ambapo kwa upande wake aliwapa ofa yake na wao walitoa ofa yao lakini baada ya hapo uongozi ulikaa kimya pasipo kuzungumzia chochote juu ya swala hilo.

Alisema kwamba anashangaa kuona uongozi unashindwa kumpa mrejesho wa kile ambacho walichozungumza kwani ilitakiwa wamjibu kama wameshindwa kumpa kiasi hicho alichohitaji ili afahamu kinachoendelea.

"Mimi nikwambie mwandishi hao viongozi walitakiwa wanipe taarifa kuhusu swala hilo waseme kwamba hawana uwezo wa ofa hiyo ili kama kuna cha ziada nami niwajibu, lakini kilichotokea baada ya hapo uongozi ulikaa kimya hadi leo hii"alisema Minziro.


Kwa upande wao uogozi wa timu ya Singida United,ulisema kwamba taarifa ambazo zinaelezwa na kocha Fredrick Minziro si taarifa za kweli,kwani bado wapo kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba.


Mkurugenzi wa Singida United,Festus Sanga alisema kwamba kwenye mazungumzo hayo bado hakuna muafaka kwani kocha Minziro ametaja kiwango kikubwa cha fedha ambacho uongozi haukuridhika na kiwango hicho.

Alisema kwamba endapo mazunguzmzo hayo yatapatiwa muafaka basi Minziro atasalia katika klabu hiyo ya mkoani Singida.

No comments