SIMBA INA HAKI YA KULIPWA KIASI CHA FEDHA CHOCHOTE WANACHOKIHITAJI KTK SWALA LA MCHEZAJI HASSANI KESSY


Wakala wa wachezaji anaetambulika na shirikisho la mpira wa miguu  dunuiani FIFA,Jamali Kisongo amesema kwamba klabu ya Simba ina haki ya kulipwa fedha kwa kiwango wanachokihitaji kutoka Yanga juu ya swala la kumuidhinisha mchezaji Hassani Kessy kujiunga na klabu ya Yanga

Kisongo amesema kwamba Hassani Ramadhani Kessy na klabu ya Yanga zimevunja mkataba wa mchezaji huyo kwa kuweza kumjumuisha katika maswala ya kiutendaji ndani ya klabu ya Yanga ilihali bado mkataba wake na klabu ya Simba haujaisha

Amesema kwamba kama inavyoelezwa na viongozi wa TFF,kua mchezaji huyo mkataba wake umemalizika june 15 mwaka huu lkn ameshangazwa na viongozi wa Yanga kuambatana nae siku ya tarehe 12 ya mwezi june katika safari ya kwenda  Uturuki kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika sambamba na kumtambulisha kwa mashabiki wa klabu hiyo katika mechi ya fainali ya kombe la FA

Aidha amedai kua Yanga huenda ikakambana na rungu zito kutoka kwa viongozi wa juu wa soka kwa kukiuka vipengele vya mkataba kwa wachezaji

Hata hivyo amewataka viongozi wa Yanga kwa sasa kuweza kuwa wapole ili waweze kuzungumza na viongozi wa Simba kupatikane muafaka wa jambo hilo.

No comments