TOTO AFRICANS YAWASIMAMISHA WACHEZAJI WANNE

Wakati nahodha wa timu ya Toto akitoweka kambini pasipo kuwepo kwa taarifa leo hii uongozi wa timu ya soka ya Toto Africans ya jijini Mwanza
umewasimamisha wachezaji wake wanne kuelekea kwenye mchezo wao wa kesho dhidi ya Simba,baada ya kubaini kuwepo na mapungufu kwa upande wa wachezaji hao.

Afisa Habari wa Toto Africans,Cuthbert Japhet alisema kwamba wachezaji hao wakiongozwa na nahodha wa timu hiyo hawatakuwemo kwenye mchezo huo wa ligi kuu ya Tanzania bara utakaopigwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Japhet alisema kwamba kiujumla maandalizi kwa upande wao yameshakamilika kila idara hivyo wanachoamini wao kuweza kuibuka na ushindi kwenye pambano hilo.

Alisema kwamba mara nyingi wanapocheza na Simba huwa wanapata matokeo mazuri hata wasipotumia kikosi cha kwanza,hivyo kukosekana kwa wachezaji hao haitakuwa sababu ya kikosi hicho kutopata matokeo mazuri.

No comments