MASHABIKI WADAI MBAO FC WAMEUZA MECHI
Baadhi ya mashabiki wa mpira wa miguu jijini Mwanza wamewalaumu baadhi ya wachezaji wa timu ya Mbao na waamuzi wa mechi ya leo kati ya Mbao na Simba kuwa wamefanya hujuma katika mchezo huo.
Mashabiki hao wamesema kwamba walishuhudia baadhi ya viongozi wa Simba wakifanya mazungumzo wakati wa mapumziko na waamuzi wakipanga kuwapa fedha ili Simba ishinde kwenye mchezo huo.
Mmoja wa mashabiki hao alisema kwamba mipango ya mwamuzi kupewa fedha kwa ajili ya kufanya hujuma ili Simba ishinde ilianzia mkoani Shinyanga kwenye mechi ya Stend United.
Alisema kwamba hata mpango wa kuongeza dakika saba za nyongeza ni shinikizo kutoka kwa uongozi wa Simba kwani kwa muda wote walikuwa wakihaha kufanikisha Simba inaibuka na ushindi.
Aidha wamedai kuwa hata wachezaji wa Mbao FC walikuwa ni wazembe kwani walikuwa hawana hata hamasa ya kuzozana na mwamuzi licha ya kutotendewa haki na mwamuzi.
Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 mbele ya Mbao FC katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara uliochezwa jijini Mwanza huku Mbao ikianza kuongoza kwa mabao 2 -0 hadi dakika ya 80 ya mchezo.

Post a Comment