MASHABIKI SITA KUTINGA MAHAKAMANI KUSIMAMISHA LIGI

Sakata la rufaa ya klabu ya Simba kwa kamati ya saa 72 imeendelea kuleta sura mpya kwa wadau wa soka hapa nchini baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa kuna baadhi ya wanachama watatu wa Kagera Sugar na watatu wa Yanga kutaka kwenda mahakama ya Kisutu siku ya jumanne kufungua kesi kupinga maamuzi ya kamati ya Saa 72.
Taarifa ambayo MWANDIKE.BLOGSPOT imeipata ambayo inasambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ni hii hapo chini.

Mashabiki wa 3 Yanga na Wa3 Kagera wanafungua kesi Mahakama ya Kisutu Jumanne ya wiki ijayo kupinga maamuzi ya Kamati ya Simba ya Saa 72. Hii ni iwapo kamati hiyo itaipoka pointi Kagera.

Wataitaka mahakama iangalie mwenendo wa chanzo cha mgogoro kulingana na tafsri za kanuni na historia ya maamuzi ya siku za nyuma ya kesi kama hizo huku shahidi muhimu akiwa mchezaji mhusika waamuzi na ripoti ya michezo yote.

 Wakienda Mahakamani Tanzania itafungiwa FIFA hivyo Yanga haitaenda Algeria na Serengeti haitashiriki Gabon. Yanga na Kagera wameridhika kwa hilo na wanafanya kwa nia njema ili kukomesha uonevu wa vilabu visivyokaribu na Malinzi. Hadidu za rejea za kesi zipo tayari na vikao na wanasheria vinaendelea hata leo.
#Haki haiombwi inadaiwa kwa njia zozote zile.

Hata hivyo MWANDIKE.BLOGSPOT inaendelea kulifuatilia swala hili kwa ukaribu ili kubaini hao mashabiki wanaotaka kwenda Mahakamani.

No comments