MBAO FC YACHUKUA MAAMUZI MAGUMU KWA WACHEZAJI WAKE

Baada ya kufungwa kwa jumla ya mabao 3-2, uongozi wa timu ya Mbao FC ya Ilemela jijini Mwanza umewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo kwa kile kilichotekea hapo jana katika mchezo wao dhidi ya Simba kwa kikosi cha timu hiyo kuruhusu magoli ya mawili ndani ya dakika chache.

Afisa Habari wa Mbao FC,Christian Malinzi alisema kwamba mbali na kuwaomba radhi mashabiki wa timu hiyo lakini kwa sasa uongozi upo kwenye kikao kizito kubaini nini kilichotekea kwa wachezaji wao kuweza kuruhusu magoli hayo mawili ambayo kwao kama uongozi una mashaka na hicho kilichotokea.

Alisema kwamba uongozi haukatai kufungwa magoli mawili kwa muda mfupi lakini je hayo magoli yamefungwa kwa namna ipi?hivyo kwa sasa kama uongozi unajalibu kuchunguza swala hilo na uongozi huo utakuwa wazi kulitolea ufafanuzi kile watakachojadili kuanzia sasa na ikibainika kuwepo kwa hujuma basi wahusika watachukuliwa maamuzi magumu.

"Baada ya kufanya kazi ambayo ulitakiwa uifanye ndani ya kazi ya mpira uliyochagua unaenda kufanya usanii sasa hiki kwa kweli kimetuhudhunisha magoli tuliyofungwa hata ukiangalia ndugu mwandishi utawaza ni juhudi ipi ambayo imefanywa kulinda hayo magoli"alisema Malinzi.

Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 mbele ya Mbao FC katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara uliochezwa jijini Mwanza huku Mbao ikianza kuongoza kwa mabao 2 -0 hadi dakika ya 80 ya mchezo.

No comments