SINGIDA UNITED WAKATAA KUFANYA USAJILI WA MSHAMBULIAJI WA AMAVUBI

Uongozi wa klabu ya Singida United,umesema kwamba kwa sasa hawajafanya mazungumzo na mchezaji yeyote wa kimataifa mbali na wale wachezaji watatu waliosajiliwa na klabu hiyo wakitokea nchini Zimbabwe.

Katibu mkuu wa Singida United,Abdulrahamani Salum Sima ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba kwa wakati huu wanamsubili kocha mkuu wa timu hiyo Hans van Der Pluijm anaetaraji kurejea siku ya tarehe 14 ya mwezi huu ili aendelee na majukumu yake ya kufanya usajili na mambo mengine.

Sima amesema kwamba hata taarifa za klabu hiyo kutaka kumsajili mshambuliaji wa Amavubi ya Rwanda Danny Usengimana kutoka timu ya Polisi,taarifa hizo si za kweli kwani uongozi haujafanya mazungumzo yeyote na mchezaji husika.

No comments