SIMBA KUISHUSHA YANGA KILELENI LEO HII

Timu ya soka ya Simba inaweza kurejea kileleni katika msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara endapo watafanikiwa kuibuka na ushindi kwenye mechi yao dhidi ya Mbao FC itakayopigwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Simba kwa sasa ana jumla ya alama 55 baada ya kushuka dimbani mara 25 ambapo leo hii wakipata ushindi watafikasha alama 58 na kuwazidi Yanga alama mbili iliyo na pointi 56 baada ya kucheza mechi 25.
Hata hivyo Yanga itakuwa na mechi ya kiporo kwani Simba itafikisha mechi 26 huku Yanga wao wakikosa kucheza mechi ya ligi kwa waki hii kutokana na ushiriki wao wa michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Mechi ya Simba na Mbao FC inataraji kuwa na ushindani mkubwa kutokana na hamasa iliyopo kwa kikosi cha Mbao pamoja na Simba ambao wanawania kuchukuwa ubingwa wa ligi kuu hiyo.

Simba itamkosa mchezaji wake mahili Abdi Banda,baada ya kusimamishwa na kamati ya masaa 72 ya TFF kwa muda usiojulikana baada ya kumpiga mchezaji wa Kagera Sugar George Kavilla.


No comments