WACHEZAJI WA YANGA WAPANDISHA KIWANGO

Kocha msaidizi wa timu ya soka ya Yanga,Juma Mwambusi amewapongeza wachezaji wake kwa kujituma zaidi tangu kipindi cha kwanza cha mchezo dhidi ya Mc Alger ya Algeria na kufanikiwa kuibuka na ushini wa bao 1-0.

Mwambusi alisema kwamba wachezaji wake wamefanikiwa kuongeza kiwango katika mechi za CAF angalau kwa asilimia 52 na katika mechi ya jana ya kombe la shirikisho barani Afrika wameonekana kucheza vizuri.

Alisema kwamba mbali na kucheza vizuri lakini waameshindwa kuzitumia nafasi za wazi ambazo kungekuwa na umakini wangefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao mengi zaidi kwani wametengeza nafasi zaidi ya sita lakini hawajazitumia vyema.

Aidha alidai kuwa kwa sasa wanayafanyia kazi mapungufu ambayo yamejitokeza kabla ya mechi ya marudiano itakayopigwa nchini Algeria ili wafanikiwe kusonga mbele ili wafuzu kwenye hatua ya makundi kwani kwa sasa mpira hauna ugenini wala nyumbani.

Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhdi ya Mc Alger,bao ambalo limefungwa na Thabani Kamusoko kwenye pambano lililochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kwa matokeo hayo Yanga inahitaji ushindi au sale yeyote ili ifanikiwe kufuzu kwenye hatua ya makundi ya kombe la shirikisho baada ya kuondoshwa katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika na timu ya Zanaco ya Zambia.

No comments