AZAM FC YAENDA TANGA KUIKABILI JKT RUVU

Kikosi cha timu ya soka ya Azam FC,leo hii kimetaraji kuelekea mkoani Tanga kwa ajili ya kujiwinda na mchezo wao wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya JKT Ruvu,mchezo unaotaraji kupigwa siku ya jumamosi katika uwanja wa Mkwakwani.

Afisa Habari wa Azam,Jafari Idd alisema kwamba baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar kikosi kilirejea siku ya jana jijini Dar es salaam na kuingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo.

Jafari Idd alisema kwamba kikosi hicho kitaelekea mkoani Tanga kwa tahadhari kubwa kwani wanaamini pambano hilo litakuwa na ushindani mkubwa kwa pande zote kwani JKT Ruvu hawapo kwenye nafasi nzuri ya msimamo wa ligi.

No comments