YANGA KAMILI KWA MAPAMBANO DHIDI YA MC ALGER

Kikosi cha timu ya Yanga kimewasili salama nchini Algeria tayari kwa mchezo wao wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya MC Alger unaotaraji kupigwa hapo kesho.

Yanga leo hii wamefanya mazoezi yao katika uwanja wa Stade 5 Julliet 1962 kabla ya kuwavaa wapinzani wao


Katibu mkuu wa klabu ya Yanga,Charse Boniphace Mkwasa amesema kikosi kimelekea nchini Algeria kwa nia moja tu ya kupata matokeo mazuri ambayo yatawawezesha kufuzu hatua nyingine.
Mkwasa Alisema kwamba anaamini pambano litakuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa pande zote kwani wapinzani wao hawatakubali kufungwa kwa mara ya pili wakiwa nyumbani,lakini hilo haliwapi hofu na watapambana hadi dakika za mwisho.
Yanga inaingia katika mchezo huo  dhidi ya MC Alger ikiwa na faida ya ushindi wa goli moja ambao waliupata hapa nyumbani,hivyo ushindi wowote ama sale utawafanya kufuzu katika hatua ya makundi kwenye mashindano hayo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya vilabu barani Afrika.


No comments