KAMATI YA SHERIA YA TFF KUJADILI UPYA RUFAA YA KLABU YA SIMBA

Kamati ya Sheria,Katiba na Hadhi za Wachezaji ya TFF,inataraji kuketi siku ya jumanne kupitia upya rufaa ya klabu ya Simba ikipinga Kagera Sugar kumchezesha mchezaji mwenye kadi tatu za njano katika mchezo wao wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Kamati ya saa 72 ya TFF,ilitoa maamuzi ya kuipa klabu ya Simba pointi tatu na magoli matatu baada ya kubaini kuwa Kagera ilimchezesha mchezaji Mohamed Fakh mwenye kadi tatu za njano.

Aidha baada ya maamuzi hayo uongozi wa Kagera Sugar uliwasilisha barua TFF,ikihitaji shirikisho la soka lipitie upya shauri hilo kwani kwa upande wao hawakubaliani na maamuzi hayo ambayo kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na mwenyekiti wa Kagera Sugar Hamisi Madaki imedai kuwa maamuzi ya kamati ya saa 72 hayakutenda haki.

MWANDIKE.BLOGSPOT leo hii imepata maelezo yanayodai kuwa  kamati ya Sheria,Katiba na Hazi za wachezaji itakutana siku ya jumanne ya tarehe 14/4/2017 katika hotel ya Protea Sea View saa nne asubuhi kujadili swala hilo.

Wanaoitajika kwenye kikao hicho ni pamoja na Joel Balisidya,Rose Msamila,Michael Ngogo,waamuzi wote waliochezesha mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara kati ya African Lyon na Kagera Sugar,wasimamizi wa mchezo huo pamoja na viongozi wa Kagera Sugar.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa kila mmoja anahitajika kufika na nyaraka alizo nazo zinazohusiana na mchezo huo na TFF itarudisha gharama za safari kwa wale wanaotoka nje ya mkoa wa Dar es salaam.

Hata hivyo MWANDIKE.BLOGSPOT ilijalibu kuwasiliana na afisa Habari wa TFF,Alfred Lucas kujiridhisha zaidi juu ya taarifa hiyo ambapo amedai kuwa yeye hajapata taarifa rasmi juu ya jambo hilo  kwa kuwa hayupo Ofisni kwa siku ya leo.

No comments