OBREY CHIRWA KUWAKOSA MC ALGER

Kikosi cha timu ya soka ya Yanga hapo kesho kinataraji kuanza safari ya kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano wa kombe la shirikisho barani Afrika dhdi ya MC Alger.

Msafara huo utakuwa na jumla ya wachezaji 20,benchi la ufundi na viongozi utaondoka hapo kesho majira ya saa 12 kwa ndege ya  shirika la ndege la Emirates kupitia Dubai.

Wachezaji watakaondoka ni makipa Deogeratuis Munishi na Beno Kakolanya.

Nafasi ya ulinzi ni pamoja na Nadir Haroub,Vicent Bossou,Juma Abdul,Andrew Vicent,Osca Joshua,Mwinyi Haji,Hassan Ramadhani na Kelvin Yondani.

Viongo ni Thabani Kamusoko,Haruna Niyonzima,Deus Kaseke,Said Makapu,Juma Mahadhi,Simon Msuva,Geofrey Mwashuiya na Emmanuel Martin.

Kwa upande wa washambuliaji ni Amisi Tambwe na Donald Ngoma.

Aidha wachezaji kama Justine Zulu,Malimi Busungu,Matheo Antony,Ally Mustapha,Pato Ngonyani,Obrey Chirwa na Yusufu Mhilu watakosa mchezo huo kwa sababu mbalimbali ambao kwa pamoja hawataambatana na wenzao.

No comments