YALIYOJIRI KWENYE KAMATI YA SAA 72

Wakati taarifa zikisambaa mitandaoni kuwa klabu ya Simba imepewa pointi tatu baada ya kushinda rufaa yao dhidi ya klabu ya Kagera Sugar kwa kumchezesha mchezaji Mohamed Fakhi mwenye kadi tatu za njano,mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo ya saa 72 ameweka bayana juu ya taarifa hizo.

Mjumbe huyo wa kamati ya utendaji ambae hakupenda atajwe jina lake ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba taarifa hizo hazina ukweli wowote kwani kamati hiyo ya saa 72 inataraji kuketi kuanzia mishale ya saa tisa alasili kwa ajili ya kuamua jambo hilo.

Alisema kwamba ni vyema wadau wa mpira wa miguu wakaiacha kamati ifanye kazi na sio kuzungumza vitu ambavyo havina ukweli wowote.

No comments