MKWASA AMVAA OBREY CHIRWA

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kwamba hawawezi kumlazimisha mchezaji Obrey Chirwa kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya MC Alger.

Katibu mkuu wa klabu ya Yanga,Charse Boniphace Mkwasa ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba Chirwa amekitaa kuambatana na timu kwa sababu zake binafsi hivyo uongozi haukuona haja ya kumlazimisha.

"Tumecheza mechi nyingi bila wachezaji muhimu na tulipata matokeo mazuri,kwa  hiyo kukataa kwake sio sababu ya timu kushindwa kupata matokeo mazuri"alisema Mkwasa.

Msafara wa wachezaji 20,benchi la ufundi na viongozi wa Yanga leo mishale ya saa 12 jioni utaanza safari kuelekea Algeria kwa ndege ya shirika la ndege la Emirates tayari kwa mchezo wa marudiano wa kombe la shirikisho barani Afrika utakaoamua mshindi atakaefuzu hatua ya makundi.

Wachezaji watakaondoka ni makipa Deogeratuis Munishi na Beno Kakolanya.

Nafasi ya ulinzi ni pamoja na Nadir Haroub,Vicent Bossou,Juma Abdul,Andrew Vicent,Osca Joshua,Mwinyi Haji,Hassan Ramadhani na Kelvin Yondani.

Viongo ni Thabani Kamusoko,Haruna Niyonzima,Deus Kaseke,Said Makapu,Juma Mahadhi,Simon Msuva,Geofrey Mwashuiya na Emmanuel Martin.

Kwa upande wa washambuliaji ni Amisi Tambwe na Donald Ngoma.

Aidha wachezaji kama Justine Zulu,Malimi Busungu,Matheo Antony,Ally Mustapha,Pato Ngonyani,Obrey Chirwa na Yusufu Mhilu watakosa mchezo huo kwa sababu mbalimbali ambao kwa pamoja hawataambatana na wenzao.

Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa mchezaji Obrey Chirwa amekataa kuambatana na wenzake ili kushinikiza uongozi umlipe malimbikizi ya mishahara yake ya miezi mitatu ambayo anaidai klabu hiyo ya Yanga.

No comments