KAGERA SUGAR WATINGA TFF,WATAKA WAPEWE POINTI ZAO

Uongozi wa klabu ya Kagera Sugar umetuma barua rasmi kwa shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF kupinga maamuzi ya kamati ya saa 72 kuipa pointi tatu na magoli matatu klabu ya Simba baada ya kushinda rufaa yao ya kupinga klabu ya Kagera Sugar kumchezesha mchezaji Mohamed Fakh akiwa na kadi tatu za njano.

Katika barua iliyosainiwa na mwenyekiti wa klabu hiyo Hamisi Madaki,inasema kwamba Kagera Sugar inapinga vikali maamuzi hayo ya kuipa Simba pointi tatu na magoli matatu,kwani kumbukumbu zao mchezaji Mohamed Fakh, hakuwa na kadi tatu kabla ya mchezo huo wa tarehe 2/4/2017,bali alikuwa na kadi mbili tu za njano alizoonyeshwa kwenye michezo yao dhidi ya Mbeya City na Majimaji ambayo ilichezwa huko nyuma.

Taarifa hiyo imeiomba TFF ifanye marejeo ya maamuzi ya rufaa iliyokatwa na Simba kwenye mchezo huo ili haki iweze kutendeka ili kulinda taswira ya soka letu.

No comments