YANGA WAIPELEKA KAMATI YA SAA 72 TAKUKURU

Uongozi wa klabu ya Yanga umetoa tahadhari kwa kamati ya masaa 72 ya TFF kuwa makini na maamuzi yao juu ya rufaa ya klabu ya Simba inayohitaji kupewa pointi tatu za mezani kwa madai kuwa timu ya Kagera Sugar imemchezesha mchezaji Mohamed Fakhi wakati ana kadi tatu za njano.

Akiongea mbele ya waandishi wa habari leo hii katika makao makuu ya klabu,mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga Salumu Mkemi alisema kwamba kamati ya utendaji ya klabu hiyo ilikaa siku ya jana kwa ajili ya kujadili maswala mbalimbali ikiwemo swala la Simba kutaka kupewa pointi za mezani.

Mkemi alisema kwamba kamati hiyo imechukua hatua ya kuwasaliana na taasisi ya kuzuia na kupanda na rushwa TAKUKURU pamoja na vyombo vingine vya sheria kwa ajili ya kuichunguza kamati ya masaa 72 kwani kuna viashiria vya rushwa ndani ya kamati hiyo.

Alisema kwamba Yanga hawana imani na kamati hiyo kwani haina usawa,ambapo amedai kuwa kamati hiyo inaundwa na zaidi ya wanachama sita wandamizi wa Simba SC na wao kama Yanga wakiwa na wanachama wawili tu.

"Kamati hii imechelewa kutoa maamuzi kwa kuandaa ripoti za uongo za michezo dhidi ya Fakhi pia tuna taarifa za kughushiwa email na nyaraka nyingine ili kuipa alama tatu Simba SC yenye zaidi ya wajumbe sita katika kamati hiyo"alisema Mkemi.

Hata hivyo amedai kuwa kamati hiyo imetoa rai kwa TFF kuunda kamati zisizo na maslahi pande yeyote ili kuleta haki katika maamuzi mbalimbali ya soka letu.

No comments