MAJIMAJI WAKO VYEMA KUWAVAA RUVU SHOOTING

Katibu mkuu wa timu ya Majimaji,Hamfrey Milanzi amesema kwamba kikosi cha timu hiyo kimejianda vizuri kuelekea kwenye mchezo wao wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Ruvu Shooting unaotaraji kupigwa siku ya jumamosi.

Milanzi alisema kwamba kwa sasa kikosi tayari kimeshawasili jijini Dar es salaam tayari kwa mechi hiyo itakayopigwa kwenye uwanja wa Mabatini uliopo mkoani Pwani.

Alisema kwamba pambano hilo ni gumu kwa upande wao kwani bado hawapo kwenye matumaini ya kusalia katika ligi kuu msimu ujao kutokana na nafasi iliyopo timu hiyo ya Majimaji huku kila timu ikidhamiria kufanya vyema ili isalie katika ligi kuu na nyingine kuwepo kwenye mbio za ubingwa.

Majimaji inashika nafasi ya tatu kutoka mwisho katika msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara wakiwa na alama 26 baada ya kucheza mechi 26.

No comments