MBAO FC YAMTUMBUA GOLIKIPA WAO

Uongozi wa klabu ya Mbao FC ya Ilemela jijini Mwanza umemsimamisha mlinda mlango wa timu hiyo Erick Ngwengwe kwa muda usiojulikana kwa tuhuma za upangaji wa matokeo kwa madai kuwa amechukuwa rushwa kwa klabu ya Simba au kuwa na mapenzi binafsi na Simba.

Afisa Habari wa Mbao FC,Christian Malinzi ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kuwa katika kikao kilichoketi siku ya jana uongozi umeamua kumsimamisha kwa muda usiojulikana ili kupisha uchunguzi zaidi juu ya kile kinachoenekana amehusika katika upangaji wa matokeo.

Malinzi alisema kwamba uongozi ulijalibu kutafuta dodosa za tuhuma hizo,umebaini kuwepo kwa viashiria vya upangaji wa matokeo ambavyo vimesababishwa na yeye kwa kuweza kuruhusu magoli ya kizembe.

Alisema kwamba kwa sasa hawawezi kumtuhumu moja kwa moja kuwa ndie aliyehusika na swala hilo ndio maana uongozi umeamua kumuondoa kambini ili kupisha uchunguzi wa kina juu ya yake.

Hata hivyo alisema kwamba ingawa hakuna taarifa ya kuhusika katika swala la kuchukua fedha lakini huenda kukawepo na mapenzi binfsi kwa mchezaji mwenyewe kuipenda timu Pinzani kwani wachezaji wengi wa Tanzania wamegawanyika katika vilabu vya Simba na Yanga.

No comments