JKT RUVU WAWASILI MKOANI TANGA KUWAVAA AZAM FC

Baada ya safari ndefu toka mkoani Kagera,kikosi cha timu ya JKT Ruvu ya mkoani Pwani tayari kimeshawasili mkoani Tanga kwa ajili ya kujiwinda na pambano lao dhidi ya Azam FC katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara unaotaraji kupigwa siku ya jumamosi ya tarehe 15 mwezi huu.

Afisa Habari wa JKT Ruvu,Costatine Masanja ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kuwa baada ya kuvuna pointi mbili katika mechi mbili walizocheza ugenini mbele ya Mwadui FC na Kagera Sugar kwa sasa kikos kinaendelea na maandalizi chini ya mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo Abdalah Kibadeni kwa ajili ya pambano hilo.

Masanja alisema kwamba wachezaji wote wako vizuri na kila mmoja ana hamasa ya kufanya vyema kwenye pambano hilo ili waweze kuinusuru timu katika janga la kushuka daraja.

JKT Ruvu kwa sasa wanaendelea kushika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara wakiwa na alama 22 baada ya kucheza michezo 26,hivyo kikosi hicho kina kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha wanasalia katika ligi kuu ya Tanzania bara msimu ujao.

No comments