YANGA KUWAFUATA MEDEAMA NA MSAFARA WA WATU 30


Kikosi cha timu ya Yanga kinataraji kuelekea nchini Ghana siku ya jumamosi ya tarehe 23/07/2016 majira ya asubuhi tayari kujiandaa na mechi yao ya kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Medeama

 Msafara wa kikosi cha Young Africans utakua na jumla ya watu 30, ambapo kati ya hao 21 ni wachezaji na viongozi 9

Yanga inaelekea kwenye mechi hiyo ikiwana na kukumbu ya kuendelea kushika nafasi ya mwisho katika msimamo wa kundi A wakiwa na alama moja baada ya kucheza mechi tatu huku kundi hilo likiongozwa na timu ya TP Mazembe yenye pointi saba bara baada ya kushuka dimbani katika michezo mitatu.


No comments