NCHEMBA ATOA ONYO KWA WANAOSHIRIKI MASWALA YA RUSHWA MICHEZONI



Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ametoa onyo kali kwa wanaoshiriki masuala ya rushwa michezoni na hasa kwenye mpira wa miguu kwa ligi za madaraja yote

Mwigulu amesema kwamba amekuwa akishangazwa na ujasiri wa watu ambao wako tayari kutoa rushwa hata kwenye timu za polisi au jeshi kwa maslahi yao ama timu fulani iweze kupata matokeo mazuri ama mabaya

Amesema kwamba kutokana na jambo hilo serikali ya awamu ya Tano itahakikisha watalidhibiti swala hilo ambalo amedai kua linarejesha nyuma maendeleo ya mpira wa miguu hapa nchini.

No comments