MAVUGU AWAACHA NJIA PANDA WEKUNDU WA MSIMBAZI SIMBA


Mshambuliaji kutoka nchini Burundi ambae anawaniwa na klabu ya Simba Laudit Mavugo inasemekana ameelekea nchini Ufaransa kwa ajili ya kwenda kufanya majaribio ya wiki mbili katika klabu ya Tours ya ligi daraja la pili maarufu kama ligue 2

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vinavyoaminika kutoka nchini Burundi vimesibitisha kuwepo kwa taarifa hiyo ya Mavugo kuelekea nchini Ufaransa kwa ajili ya majaribio ya wiki mbili

Awali kumekuwepo na taarifa kwamba mshambuliaji huyo yuko mbioni kusaini kandarasi ya kuitumikia Simba na msimu uja lkn kutokana na majaribio hayo huenda ikawa ni vigumu kwa mchezaji huyo kujiunga na Simba kwa sababu dirisha la usajili wa hapa nchini linatarajiwa kufungwa hivi karibuni

Hii ni mara ya pili mchezaji huyo kuhitajika na Simba kwani msimu uliopita uongozi wa Simba ulishindwana nae mara baada ya Timu ya Vitaro ya Burundi kuhitaji fedha nyingi za usajili kwa ajili ya kuvunja mkataba licha ya viongozi wa Simba kukubaliana na mchezaji na kumpa kiasi cha fedha

No comments