JOHN BOKO KUENDELEA KUSALIA AZAM FC


Uongozi wa Azam FC umesema kwamba bado utaendelea kua na nahodha na mshambuliaji John Rapahael Bocco katika kikosi cha timu hiyo baada ya kocha kutoka nchini Hispania Zeben Hernandez kupendezwa na kiwango cha mchezaji huyo

Afisa habari wa Azam FC, Jaffary Iddy amesema kwamba awali kulikuwepo na taarifa za mchezaji huyo kuhitajika na baadhi ya timu kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa lkn baada ya kuzungumza na kocha mkuu ikaonekana mchezaji huyo bado anahitajika kusalia Chamzi

Aidha amesikitishwa na taarifa za baadhi ya wadau wa soka wanaosema kwamba mchezaji huyo ni miongoni mwa wachezaji watakaochwa kwa kua hayumo kwenye program ya kocha mkuu Zeben Hernandez

No comments