MALINZI AFUNGUA KOZI YA UKOCHA LESENI A


Raisi wa shirikisho la mpira wa miguu wa hapa nchini TFF,Jamali Malinzi amefungua rasmi kozi ya ukocha leseni A inayotambulika na shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF ambayo inaendeshwa na wakufunzi wa CAF,Sundy Kayuni na Salum Madadi inayojumuisha makocha 20 kutoka vilabu vya ligi kuu na madaraja mengine akiwemo Mecky Mexme ambae ni kocha wa Kagera Sugar kwa sasa pamoja na Denisi Kitambai kocha aliemaliza mkataba wake katika klabu ya Azam FC aliyekua kocha msaidizi na wengineo

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii,Malinzi amewataka makocha hao kutumia elimu watakayoipata kuweza kuleta tija ya soka la hapa nchini na sio kuishia kuviweka kabatini vyeti ambavyo watavipata

Amesema kwamba bado kuna kazi kubwa ya kuweza kupata makocha wengi ambao watakizi haja ya kuzifundisha timu za Tanzania hivyo mipango yao TFF,ni kuona wanafanya jitihada kubwa ya kuendelea kufanya njia mbalimbali za kuongeza idadi ya makocha kupitia kozi mbalimbali zinazotambulika na CAF kwa kua Tanzania ina idadi ndogo ya makocha ukilinganisha na nchi za wenzetu zenye makocha wengi ambao wanafanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali.

No comments