MFUNGAJI BORA WA LIGI YA ZIMBABWE ATUA AZAM


NYOTA wa Kimataifa ya Zimbabwe, Bruce Kangwa, ametua nchini jioni ya leo tayari kabisa kufanya majaribio ya kujiunga na Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC.
Kangwa anatokea kwa vinara wa Ligi Kuu nchini humo Highlanders FC na mpaka sasa ligi hiyo ikiwa mapumzikoni kufuatia kumaliza mzunguko wa kwanza, amefanikiwa kuwa kileleni kwa ufungaji bora akiwa na mabao saba.
Mzimbabwe huyo ameshachezea timu yake ya Taifa mechi 20 na mpaka sasa yupo kwenye kikosi hicho na anamudu kucheza nafasi tatu tofauti uwanjani, beki wa kushoto, winga wa kushoto na mshambuliaji.

No comments