NCHEMBA AKASIRISHWA NA WANAMICHEZO WASIO TAMBUA UMUHIMU WA BENDERA YA NCHI
Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu
Nchemba amewataka viongozi wa vilabu vya ligi kuu pamoja na shirikisho la mpira
wa miguu hapa nchini TFF,kuweza kupanga utaratibu wa kuwaelimisha mashabiki wao
kuheshimu bendera ya Taifa pindi klabu ama timu za Taifa zinapocheza katika
michuano mbalimbali ya kimataifa
Nchemba ameyasema hayo kufuatia kutoridhishwa na baadhi
ya mashabiki wa hapa nchi kuweza kuzomea wakati bendera ya Tanzania
inapandishwa katika mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika kati ya Yanga
na TP Mazembe mechi iliyopigwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam
Amesema kwamba ni vyema mashabiki wakatambua umuhimu wa
bendera ya nchi kwani wazee wetu walipigania kwa nguvu kubwa kupata uhuru wa
Tanzania,hivyo inashangaza kuona mtanzania unazomea wakati bendera yako ya nchi
inapandishwa huku ukishangilia bendera ya nchi nyingine inapopandishwa
Hata hivyo amewataka watanzania kuiga mfano wa mchezaji Mbwana Samata ambae alionyesha uzalendo wa nchi yake wakati timu yake za zamani ya TP Mazembe ilipotwaa taji la ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Afrika ambapo baada ya mechi kumalizika alionekana kubeba bendera ya Tanzania mbele ya uma wa watu kutoka nchi tofauti.
Post a Comment