WAKENYA WAMFUKUZA KOFFI OLOMIDE

Mwanamuziki Koffi Olomide ambae ni msanii maarufu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amefukuzwa nchini Kenya, baada ya kukamatwa hapo jana kwa kumpiga teke mnenguaji wake wa kike katika uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.
Mkanda wa Video uliosambaa katika mitandao ya kijamii pindi tu baada ya Koffi mwenye umri wa miaka 60, kumshambulia mwanadada huyo ulilaaniwa na wakenya kupitia mitandao ya kijamii hasa Twitter lakini pia wabunge kwa nyakati tofauti
Olomide alikamatwa jana usiku na polisi baada ya kumaliza mahojiano maalum katika kituo kimoja cha Televisheni nchini humo na kuzuiwa katika kituo cha polisi katika uwanja wa ndege.
Hii sio mara ya kwanza kwa nguli  huyo wa muziki ambaye kwa sasa anafahamika kwa wimbo wake maarufu wa “Ekotite” unaotamba sehemu mbalimbali kukabiliwa katika hali hii ya kuwashambulia watu wakiwemo wanahabari.
Kutokana na jambo hilo la Kurudishwa nyumbani jijini Kinshasa kunamaanisha kuwa tamasha lake lililotarajiwa kufanyika leo Jumamosi jijini Nairobi halitafanyika tena hivyo mashabiki ambao walikua na shauku ya kushuhudia tamasha hilo wamekosa fursa ya kuona burudani kutoka kwake.

No comments