JUMA ABDUL ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA LIGI KUU YA TANZANIA BARA


Beki wa Yanga, Juma Abdul Jaffar Mnyamani ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2015/2016.
Katika sherehe za utoaji wa tuzo zilizofanyika katika ukumbi wa Double Tree Hotel By Hilton, Masaki, Dar es Salaam

Abdul amewashinda beki mwenzake, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ wa Simba na kiungo wa Mtibwa Sugar, Shizza Kichuya
Akiongea katika sherehe hizo mara baada ya kutangazwa kua yeye ndie mshindi kwa upande wake ameweza kufurahia kupata tuzu hiyo ambapo amesema kwamba mafanikio hayo kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na kocha mkuu wa klabu ya Yanga,Hans Pluijim pamoja na kujituma kwake katika mazoezi

Amesema kwamba tuzo hiyo imempa chachu ya kuendelea kufanya vizuri katika msimu ujao kwani dhamira yake ni kuona anafika mbali kwenye maisha ya soka


ORODHA KAMILI YA WASHINDI WA TUZO
@@@@@

Mchezaji bora-Juma Abdul
Kocha bora- Hans Van Pluijim
Mchezaji bora wa kigeni-Thabani Kamusoko
Golikipa bora-Aishi Manura
Mfungaji bora-Amiss Tambwe
Mchezaji bora chipukizi-Mohamed Hussein
Goli bora la msimu-Ibrahim Ajibu
Timu yeneye nidhamu-Mtibwa
Mwamuzi bora-Ngole Mwangole
Mabingwa-Yanga
Washindi wa pili-Azam
Washindi wa tatu-Simba
Washindi wa nne- Tza Prison

No comments