CAF YAPATA MDHAMINI MPYA

Shirikisho la Soka barani Africa (CAF) limepata mdhamini mpya baada ya kumalizika kwa mkataba wake na kampuni ya mawasiliano ya Orange.
Orange imekuwa mdhamini mkuu wa mashindano makubwa ya CAF kwa miaka minane tangu 2009.
Kabla ya hapo, kampuni nyingine ya mawasiliano ya MTN ndiyo iliyokuwa mdhamini kwa miaka minne.
Sasa, mdhamini mpya atakuwa kampuni ya mafuta na gesi ya Total kutoka Ufaransa.
Kampuni hiyo itaanza kwa kudhamini michuano ya Kombe la Taifa Bingwa Afrika mwaka 2017 ambayo itaandaliwa nchini Gabon.
Thamani ya mkataba huo haijafichuliwa.

No comments