BUKINA FASO WAHAMA MJI BAADA YA KUTOPATA USHIRIKIANO KUTOKA MRFA


Uongozi wa timu ya Bukina Faso ya mkoani Morogoro umesema kwamba timu hiyo kwa sasa imehamishiwa katika wilaya ya Kilosa baada ya kuona hawapati ushirikiano wa kutosha kutoka kwa viongozi wa soka wa chama cha mkoa wa Morogoro MRFA

Akiongea na Mwandike.blogsport,katibu mkuu wa timu hiyo Gosbarth Isack amesema kwamba msimu ujao mechi zao zote za nyumbani watachezea Kilosa baada ya kuona huko wanasaminiwa tofauti na walivyokua mjini ambapo wamekua hawapati ushirikiano mzuri 

Amesema kwamba msimu uajo wana matumaini ya kufanya vizuri katika ushiriki wa michezo ya ligi daraja la kwanza na kufanikiwa kupata nafasi ya kucheza ligi kuu ya Tanzania bara 

No comments