TELELA MBIONI KUREJEA DARASANI


Meneja wa mchezaji Salum Telela,Fadhili Shilungushela amesema kwamba kuna uwezekano mkubwa wa mchezaji huyo  kurejea darasani kuendelea na masomo baada ya kutopata ofa nzuri kutoka kwa timu mbalimbali

Shilungeshela amesema kwamba hadi sasa bado hakuna ofa iliyowasilishwa kwao na ifikapo tarehe 25 kama hakuna timu ambayo imejitokeza basi atarejea darasani kuendelea na masomo

Hata hivyo amekanusha taarifa ambazo zinasema kua wao wanahitaji kiasi kikubwa cha fedha,ambapo amedai kua swala hilo halipo kwani hakuna klabu iliyoweza kutaja dau la kumsajili

No comments