HASSANI KESSY AWAINGIZA KWENYE MATATIZO MAZITO YANGA


Wakala wa wachezaji anaetambulika na shirikisho la mpira wa miguu  dunuiani FIFA,Jamali Kisongo amesema,Yanga huenda wakakumbana na adhabu kali kutoka shirikisho la mpira wa miguu barani Afika CAF,kwa kuweza kukiuka taratibu za mikataba kwa wachezaji baada ya kuanza kumuhusisha mchezaji Hassani Kessy katika maswala ya kiutawala wakati bado ana mkataba na klabu ya Simba

Kisongo amesema kwamba Hassani Ramadhani Kessy na klabu ya Yanga zimevunja mkataba wa mchezaji huyo kwa kuweza kumjumuisha katika maswala ya kiutendaji ndani ya klabu ya Yanga ilihali bado mkataba wake na klabu ya Simba haujaisha

Amesema kwamba kama inavyoelezwa na viongozi wa TFF,kua mchezaji huyo mkataba wake umemalizika june 15 mwaka huu lkn ameshangazwa na viongozi wa Yanga kuambatana nae siku ya tarehe 12 ya mwezi june katika safari ya kwenda  Uturuki kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika sambamba na kumtambulisha kwa mashabiki wa klabu hiyo katika mechi ya fainali ya kombe la FA

Hata hivyo amewataka viongozi wa Yanga kwa sasa kuweza kuwa wapole ili waweze kuzungumza na viongozi wa Simba kupatikane muafaka wa jambo hilo kwani endapo kama viongozi wa Simba watakwenda mbele zaidi basi kuna kila dalili ya Yanga kukumbana na adhabu nzito.

No comments