MAHAKAMA YAFUTA UCHAGUZI WA STEND UNITED


Mahakama imefuta uchaguzi wa wanachama wa Stend United ambao ulifanyika june 26 mwaka huu ambao unatambuliwa na shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF

Akiongea na Mwandike.blogsport mmoja wa viongozi wa Stend  Kampuni ambae hakupenda jina lake litajwe amesema kwamba taarifa zilizopo ni kwamba mahakama imefuta uchaguzi huo na imemkamata rasmi Mbasha Matutu ambae ni mwakilishi wa TFF mkoa wa Shinyanga na imempiga faini ya shilingi laki tano

Hata hivyo uongozi Stend Kampuni ambao unaongozwa na mtendaji mkuu,Jonas Tiboroha umewasilisha vielelezo vyao vya kupinga kupokwa timu kwa baraza la michezo BMT wakidai TFF imekiuka utaratibu wa timu hiyo kwa kuweza kuwatambua wanachama ambao si wa Stendi United.

No comments