TP MAZEMBE YATANGULIZA MGUU MMOJA KATIKA HARAKATI ZA KUTINGA HATUA YA NUSU FAINALI YA MICHUANO YA KOMBE LA SHIRIKISHO


Timu ya TP Mazembe imetanguliza mguu mmoja mbele katika harakati za kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika baada ya mechi yao dhidi ya Mo Bejaia kumalizika bila kufungana

TP Mazembe wakicheza ugenini nchini Algeria wamefanikiwa kujikusanyia alama moja ambayo inapelekea kufikisha alama saba baada ya kucheza michezo mitatu na kuendelea kuongoza msimamo wa kundi [A]

Matokeo hayo yanaendelea kuididimiza timu ya Yanga ambayo ipo mkiani mwa kundi hilo wakiwa na alama moja katika jitihada zake za kutinga hatua ya nusu fainali kwani Mo Bejaia imejikusanyia pointi moja na kufikisha alama tano hivyo angalau kuonyesha matumaini ya kutinga nusu fainali


No comments