HASSANI KESSY HATARINI KUTOITUMIKIA YANGA MSIMU UJAO WA LIGI KUU YA TZ BARA



Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limesema kwamba halitaweza kumuidhinisha mchezaji Hassan Ramadhani Kessy kujiunga na klabu ya Yanga hadi hapo watakapopata barua ya idhini kutoka kwa timu ya Simba

Ofsa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba shirikisho halitachukua uamuzi wa kumuidhinisha Kessy kujiunga na Yanga ksb kuna vipengele vya kimkataba Kessy amevikiuka ikiwemo swala la kujihusisha na klabu ya Yanga wakati bado amekua hajamaliza mkataba wake 


Amesema kwamba TFF,imelifahamu jambo hilo baada ya mchezaji kuambatana na Yanga kuelekea nchini Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya kujiwinda na michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika pamoja na kujihusisha na viongozi wa Yanga katika mechi ya Yanga na Azam kwenye fainali ya kombe la FA huku mkataba wake ukiwa bado haujaisha

Lucas amesema kwamba Mkataba wa Kessy umeisha siku ya tarehe kumi na tano ya mwezi wa sita lkn mchezaji amekua akijihusisha na timu yake mpya kabla ya tarehe hiyo

Hata hivyo amewataka viongozi wa Yanga kuweza kukaa pamoja na Simba kwa ajili ya kukubaliana kwa jambo hilo ili mwisho wa siku kupatikane muafaka kamili

No comments