MALALE HAMSINI KURITHI MIKOBA YA KIBADENI


Maafande wa timu ya JKT RUVU ya Kibaha mkoani Pwani wamesema kwamba kwa sasa wapo katika mazungumzo na kocha wa timu ya JKU ya visiwani Zanzibar Malale Hamsini kwa ajili ya kurithi mikoba ya Abdalah Kibadeni

Katibu mkuu wa klabu hiyo,Ramadhani Madoweka amesema kwamba kwa sasa uongozi upo kwenye mazungumzo na kocha huyo aliyewai kuzifunfisha timu mbili tofauti kwa msimu mmoja na mazungumzo yamefikia katika hatua nzuri

Amesema kwamba kwa sasa kocha huyo bado ana mkataba na timu ya JKU lkn kilichopo kwa sasa ni viongozi wa timu hiyo wanaendelea na mazungumzo kwa ajili ya kuvunja mkataba wake

Hata hivyo amesema kwamba kuhusiana na Abdalah Kibadeni yeye amepewa jukumu la kua mkurugenzi wa ufundi wa maafande hao ambao msimu uliopita hawakufanya vizuri katika baadhi ya michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara.

No comments