MANARA AELEKEA NCHINI INDIA KWA MATIBABU YA JICHO


Mkuu wa idara ya habari na mawasilino wa klabu ya Simba Haji Sunday Manara ameondoka nchini kuelekea India kwa ajili ya matibabu ya jicho lake la kulia ambalo limepoteza uwezo wa kuona.

Haji ameondoka nchini usiku wa kuamkia hii leo huku akiwa na matarajio makubwa ya kupatiwa tiba kamili atakapofika nchini India kwa kumtanguliza mwenyezi Mungu katika azma hiyo.

Akizungumza kabla ya kuanza safari hiyo, Manara aliwashukuru wale wote waliofanikisha safari yake ya matibabu na amewasihi kuendelea kumuombea kwa mwenyezi mungu katika kipindi hiki ambacho atakuwa akifanyiwa matibabu.


No comments