MTIBWA SUGAR WAKILI KUMSAJILI HASSAN DILUNGA

Uongozi wa timu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani mkoani Morogoro umethibitisha kukamilisha usajili wa mchezaji Hassani Dilunga aliyekuwa anaitumikia timu ya JKT Ruvu ambayo imeshuka daraja.

Afsa Habari wa Mtibwa Sugar,Tobias Kifaru alisema kwamba,Dilunga anakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na klabu hiyo baada ya awali kukamilisha usajili wa wachezaji watano ambao anaamini watakuwa na msada mkubwa katika timu.

Dilunga amesaini kandarasi ya miaka miwili kwa ajili ya kuwatumikia wakata miwa hao wa Manungu.

No comments