AFYA YA RAIS WA SIMBA HALI TETE,MAHAKAMA YASHINDWA KUWASOMEA MAELEZO YA AWALI

Na Unique Maringo
Mahakama ya Hakimu mjazi kisutu,imeshindwa kuwasomea maelezo ya awali viongozi wa Simba kwakua Rais wa clabu hiyo Evans Aveva anaumwa na amelezwa ktk hospital ya Taifa ya Muhimbili.

Katika shauri hilo Aveva anashtakiwa pamoja na makamu Rais Godfrey Nyange maarufu kaburu katika makosa mbali mbali ya kugushi na kutakatisha fedha.

Mbele ya Hakimu mkuu mkazi ktk mahakama ya hakimu mkazi kisutu Thomas Simba,wakili Wa takukuru Leonard Swai ameeleza kuwa shauri hililo limekuja kwa ajilili ya usikilizwaji Wa awali,hata hivyo ameeleza kuwa Aveva hakuweza kufika mahakamani kawsababu hali yake ni mbaya na amelazwa muhimbili,naakaiomba mahakama itaje tarehe nyingine,ambapo hakimu amekubaliana na maombi hayo,nakuahirisha shauri hilo hadi Apr 25 2018.
Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka matano ya uhujumu uchumi ikiwemo kughushi,kuwasilisha nyaraka ya uongo na utakatishaji fedha ambazo ni dola za Marekani (USD) 300,000.

No comments