MAYANGA AKASIRISHWA NA MATOKEO YA TAIFA STARS

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars,Salum Mayanga amesema kwamba matokeo yaliyopatikana leo hii si matokeo mazuri kwa timu ya Taifa kwani wameweza kulazimishwa sale ya kufungana kwa bao 1-1 dhidi ya Rwanda katika mchezo wa kusaka tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani.

Mayanga alisema kwamba matatizo yalijitokeza baaada ya kuruhusu goli la mapema ambalo liliwapa faida wapinzani wao na kupelekea kucheza kwa kujiangusha zaidi kwa wachezaji wa Rwanda.

Alisema kwamba siku ya jumatatu anataraji kuanza maandalizi na kikosi hicho kwa ajili ya kujiwinda na mchezo wa marejeano utakaopigwa nchini Rwanda ambapo anaamini bado Stars ina nafasi kubwa ya kufuzu katika hatua nyingine.

Katika mchezo wa leo hii uliochezwa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza,bao la kusawazisha la Taifa Stars limefungwa na nahodha wa timu hiyo Himid Mao kwa mkwaju wa penati.

No comments