BUSUNGU AJIUNGA RASMI NA LIPULI FC

Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Yanga Malimi Busungu amejiunga na klabu ya Lipuli ya mkoani Iringa baada ya leo hii kusaini mkataba wa mwaka mmoja kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo iliyopanda daraja msimu huu.

Busungu amesaini mkataba huo akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na klabu ya Yanga kumalizika na uongozi wa Yanga ulikuwa hauna haja ya kumuongezea mkataba mpya.

Awali Busungu alikuwa anawindwa na klabu mbalimbali ikiwemo Ndanda ambao nao kwa siku ya jana walikuwa wana haha kwa udi na uvumba kutaka saini yake.

Busungu hakuwa na msimu mzuri katika klabu ya Yanga,baada ya kushindwa kupata namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza.

No comments