YANGA WAITAKA TFF,BODI YA LIGI NA WADHAMINI KUWAOMBA RADHI

Uongozi wa timu ya Yanga umelitaka shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,Bodi ya Ligi na wadhamini wa ligi kuu ya Tanzania bara kuwaomba radhi kwa kitendo chao cha kushindwa kuwapa mwaliko wa kuhudhuria katika hafla ya utoaji wa vifaa kw timu za ligi kuu.

Mjumbe wa kamati ya utendaji,Salum Mkemi,alisema kwamba kitendo walichofanyiwa si cha kiungwana hata kidogo hasa ukizingatia na ukubwa wa timu yenyewe ya Yanga.

Alisema kwamba Yanga ndio bingwa mtetezi wa ligi kuu hivyo kutoitwa kwa viongozi wa klabu hiyo ni zarau kubwa kwa upande wao.

Aidha aliongeza kuwa anashangaa kuona mpinzani wao katika soka la bongo ndio anabeba majukumu ya Yanga.

Katika utoaji wa vifaa hivyo,afsa Habari wa Simba,Haji Manara ndie alichukua jukumu la kuiwakilisha Yanga wakati wa ugawaji wa vifaa hivyo.

No comments