MAHAKAMA YAUTAKA UPANDE WA SERIKALI KUONGEZA JUHUDI SHITAKA LA VIONGOZI WA SIMBA

NA UNIQUE MARINGO
Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu imeutaka upande wa serikali katika kesi ya kutakatisha fedha na kugushi inayomkabili Rais wa  Klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake Godfrey Nyange `Kaburu` kuongeza juhudi ili wakamilishe upelelezi.

Wakili wa serikali Peter Vitalis na Mwendesha mashtaka wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru  
Leonard Swai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo pado haujakamilika.

Wakili upande wa utetezi Philemon Mtakyamirwa amedai kuwa hii ni mara ya nne waanambiwa upelelezi haujakamilika na kwamba upande wa mashtaka utambue kuwa hao ni viongozi wa kubwa na shughuli za klabu zimesimama.

Amedai kuwa upande wa mashtaka uwe siriazi na shauri hilo kwani wateja wake wako ndani na kosa linalowakabili halina dhamana.

Swai amedai kuwa vitu vya kugushi vinahitaji mchakato mrefu kidogo ili kukamilisha na kwamba kutaka upelelezi kukamilika kwa haraka ni kuisumbua mahakama na kwamba utaratibu wa kesi ni siku 14.

Swai ameomba muda ili kuendelea na upelelezi wa shauri hilo.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili  ,Hakimu Nongwa amesema kesi ya kugushi upelelezi huwa ni mgumu na kesi hiyo haipati hati ya siku 60,na kugushi huwa kuna dhamana lakini kwasababu kuna makosa mengine ambayo hayana dhamana washtakiwa wataendelea kukaa ndani.

Alisema kuwa ombi la upande wa utetezi lina mashiko na kwamba upande wa mashtaka waongeze juhudi katika upelelezi.

Shauri hilo lmeahirishwa hadi Agosti 7 mwaka huu kwaajili ya kutajwa

Evans Elieza  Aveva na makamu wake, Geofrey wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha USD 300,000.

No comments