AISHI MANULA KUUNGANA NA SIMBA HAPO KESHO

Golikipa wa kimataifa wa Tanzania Aishi Salum Manula kesho tarehe moja,anatarajiwa kujiunga rasimi na kambi ya klabu ya Simba iliopo Eden Vale Johannesburg, nchini Afrika kusini.

Manula ambae ndio Golikipa namba moja wa nchi hii ameshamalizana kila kitu kuhusu kujiunga na klabu ya Simba,na ameahidi kuwapa furaha wanachama na washabiki wa klabu hiyo,sambamba na kuisaidia klabu kushinda mataji itakayowania msimu huu.

Wakati huo huo kesho timu ya Simba inatarajiwa kucheza mechi ya kwanza ya maandalizi ya msimu dhidi ya mabingwa wa zamani wa Afrika Orlando Pirates ya nchini Afrika kusini.

Orlando ambayo ndio klabu maarufu zaid nchini humo,imeahidi kushusha silaha zake zote muhimu ili kuwapa maandalizi ya kutosha Simba,Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwenye dimba la Orlando liliopo jijini Johannesburg.

Mechi nyingine ya mwisho itakayochezwa na Simba nchini humo itapigwa siku ya Alhamis ya wiki hii dhidi ya mabingwa wa soka nchini humo kwa sasa Bidvest

No comments