SIMBA WAMATANGAZA RASMI HARUNA NIYONZIMA

Uongozi wa klabu ya Simba ya jijini Dar es salaam,leo hii umetangaza rasmi kumalizana na mchezaji wa zamani wa timu ya Yanga Haruna Niyonzima baada ya uongozi wa klabu hiyo kudai kuwa taratibu za usajili wake zimeshamalizika na sasa ni mchezaji rasmi wa klabu hiyo.

Mkuu wa idarara ya Habari na mawasiliano wa klabu ya Simba,Haji Manara amesema kwamba kwa sasa Niyonzima na mchezaji wa Simba na wala si jambo la kificho kwa kipindi hiki kwani uongozi  tayari umeshakamilisha taratibu zote za usajili wake.

Manara amedai kuwa mchezaji huyo anataraji kuwasili hapa nchini wakati wowote kuanzia sasa na ni miongoni mwa wachezaji watakaokuwepo kwenye tamasha la Simba Day linalotarajiwa kufanyika agost 8 mwaka huu.

No comments